Wazazi wa AKA wagoma mtoto wao kuandikwa kitabu

Wazazi wa AKA wagoma mtoto wao kuandikwa kitabu

Wakati Melinda Ferguson akijiandaa kuandika kitabu kitakachozungumzia maisha ya mahusiano kati ya AKA na aliyekuwa mpenzi wake Anele, familia ya marehemu AKA, Tony na Lynn Forbes imetoa taarifa kuwa hawahusiki na kitabu hicho kwani walikataa kuchangia chochote kinachomuhusu mtoto wao huku wakidai kuwa uchapishwaji wa kitabu hicho ni kwa ajili ya fursa.

Kitabu hicho kipya cha Melinda kilichopewa jina la ‘When Love Kills: The Tragic Tale of AKA na Anele’ kinatarajiwa kuachiwa rasmi katika maadhimisho ya miaka mitatu ya kifo cha Anele Tembe miezi kadhaa ijayo.

Aidha kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeripoti kuwa familia ya Anele imemruhusu na kutoa Baraka zote kwa Ferguson kuandika kitabu hicho huku familia ya Forbes ikigoma kutoa ushirikiano.

Hata hivyo baada ya kuwa na mtafaruku kupitia mitandao ya kijamii mwandishi Melinda Ferguson ametetea hoja yake ambapo ameeleza kuwa nia ya kutoa kitabu hicho ni kufichua matatizo baina ya watu wawili walioingia kwenye uhusiano wa kimapenzi wenye sumu (Toxic Love).

Ikumbukwe kuwa AneleTembe alifariki Aprili 2021 akiwa na miaka 22 baada ya kuanguka katika moja ya ghorofa lililopo Cape Town, huku ‘rapa’ Kiernan Forbes (AKA) akifariki Februari 10 baada ya kupigwa risasi nje ya mgahawa uliyopo Durban.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags