Wauguzi washtakiwa kwa kuchukua viungo vya watoto

Wauguzi washtakiwa kwa kuchukua viungo vya watoto

Wauguzi wanne kutoka mkoani Tabora wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuchukua viungo vya watoto mapacha huku kitendo hicho kinahusishwa na uchawi.

Afisa wa mkoa ameeleza kuwa kamati iliyoundwa kuchunguza tukio hilo iligundua kuwa miili ya mapacha hao waliozaliwa kabla ya wakati wao ilikuwa imeharibika.

Mama mwenye watoto hao alikuta macho ya watoto wake yametobolewa na sehemu ya ngozi yao ikiwa imetolewa kwenye paji la uso.

Lakini wauguzi hao waliipotosha kamati ya uchunguzi kwa madai ya uwongo kwamba miili hiyo ilihifadhiwa katika wodi ya wazazi wakati, ilipatikana katika chumba cha wauguzi.

Aidha mkuu wa mkoa wa Tabora, Batilda Buriani alisema wauguzi hao ambao wako chini ya ulinzi wamesimamishwa kazi.

Ripoti inaeleza kuwa mapacha hao walifariki dunia kutokana na ukosefu wa huduma za watoto wachanga, ambazo hazikupatikana katika kituo walichozaliwa.

Chanzo BBC


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post