Watumiaji tovuti za Mwananchi kuchangia fedha kidogo kusoma baadhi ya habari

Watumiaji tovuti za Mwananchi kuchangia fedha kidogo kusoma baadhi ya habari

Mhariri Maudhui Mtandaoni wa wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Zourha Malisa amesema kupitia mabadiliko yanayofanywa na kampuni hiyo, watumiaji wa tovuti za Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen sasa watakuwa wakichangia kiasi kidogo cha fedha ili kusoma habari zote za kina ikiwamo maudhui maalumu (Prime content).

Ili kufanya hivyo, mtumiaji wa tovuti hizo atatakiwa kulipia Sh500 kwa siku, Sh3,000 kwa wiki, Sh15,000 kwa mwezi na Sh91,000 kwa mwaka mzima.

“Tunapatikana mitandaoni kila siku, siku ambazo hujapata gazeti la The Citizen katika nakala ngumu utalipata mtandaoni na huko tunaongeza thamani katika habari zetu kwa kuweka video na infographics ambavyo ingekuwa ngumu kuvipata katika gazeti,” amesema Malisa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags