Tumezoea kuona mashindano mengi yakufurahisha na kuburudisha lakini kwa hili linaweza kuwa ndiyo shindano la kushangaza zaidi la watu wanaowania taji la raia mvivu zaidi linalofanyika kila mwaka kaskazini mwa Montenegro.
Shindano hilo ambalo lilianza siku zaidi ya 20 zilizopita washiriki wameendelea kukaza buti ili kutaka kuvunja rekodi hiyo ambapo mwaka jana rekodi imevunjwa kwa saa 177 huku mpaka sasa washiriki wameendelea kulala chini kwa zaidi ya saa 400
Aidha sheria kuu katika shindano hilo ni kusimama au kukaa kunachukuliwa kama sababu ya kushindwa shindano hilo lakini washiriki wanaruhusiwa kuwa na dakika 10 kila baada ya saa nane za kwenda chooni.
Ikumbukwe tuu Shindano hilo lilizinduliwa katika nchini Adriatic miaka 12 iliyopita ili kuweka mzaha wa hadithi maarufu inayowataja watu wa Montenegro kuwa ni wavivu. Mshindi wa shindano hilo atapewa Euro 1000 sawa na Tsh 2.68 milioni.
Leave a Reply