Watu wamiminika kuchangia matibabu ya Professor J

Watu wamiminika kuchangia matibabu ya Professor J

Huko mitandaoni kinachoendelea kwa sasa ni namna ambavyo watu wanahamasishana kutoa michango ya matibabu ya msanii wa hip hop Professor J ambaye kwa sasa amelazwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.

Miongoni mwa watu walioguswa kushirki katika mchakato wa kusaidia kuirejesha afya ya Professor J katika hali yake ya kawaida ni Mkurugenzi wa Clouds Media Joseph Kusaga ambaye kwenye mshahara wake ametoa kiasi cha Milioni mbili kama mchangio wake wa kusaidia matibabu ya msanii huyo.

Viongozi wengine waliotoa mchango wao ni Meya wa jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, Waziri wa Maji Jumaa Aweso na watanzania mbalimbali wanaoendelea kutuma michango yao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu wa Professor J, wameeleza kuwa msanii huyo ni mgonjwa yapata wiki 3 sasa akiendelea na matibabu hospitalini MUhimbili chini ya uangalizi maalum wa kitabibu.

Wameeleza ni jambo la kutia moyo kwamba anaendelea vizuri ingawa kwa kasi ya taratibu hivyo wamewaomba watanzania kuendelea kumuombea ili apone na kurejea kwenye hali yake ya kawaida.

“Kwa kuheshimu misingi ya ‘right to privacy’ kwa sasa imeshauriwa na familia kutoweka hadharani tatizo linalomsumbua, muda ukifika na familia ikawa tayari basi mtajulishwa anasumbuliwa na nini,” walieleza ndugu hao

Kama mdau mkubwa wa muziki hapa nchini wewe uliyesoma story hii pia unaalikwa kumsaidia Professor J hivyo mchango wako wa sala, hali na mali ni muhimu mno katika hili.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags