Watatu wajeruhiwa wakati lil Baby akirekodi video

Watatu wajeruhiwa wakati lil Baby akirekodi video

Vijana wa kiume watatu wameripotiwa kujeruhiwa kwa kupigwa risasi katika eneo la Dixie Marekani wakati mwanamuziki Lil Baby akiwa ana-shoot video ya ngoma yake mpya.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea siku ya jana Jumanne Mei 14, wakati msanii huyo akishuti video ya wimbo wake, huku ‘timu’ ya mwanamuziki huyo ikitoa neno kuwa haihusiki na ufyatuaji huo wa risasi.

Aidha maafisa wa APD waliripoti kuwa wanaume hao watatu waliojeruhiwa hawakuwa sehemu ya ‘timu’ ya Lil Baby lakini wanaamini kuwa aliyetekeleza tukio hilo alikuwa miongoni mwao, huku akiwataka wananchi kutulia na kusubiri majibu ya uchunguzi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post