Watakaokula hadharani wakati wa mfungo wataadhibiwa

Watakaokula hadharani wakati wa mfungo wataadhibiwa

Polisi wa Kiislamu katika jimbo la Kano, kaskazini mwa Nigeria wametumwa misikitini ili kuhakikisha usalama wa maisha na mali katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kufuatia taarifa kutoka katika vyombo vya habari, jeshi la polisi la kidini, linalojulikana kama Hisbah Board, lilionya kwamba wale wanaojihusisha na maovu ya kijamii katika mwezi huo mtakatifu wataadhibiwa.

“Baadhi ya vijana wanaokula hadharani wakati wa mfungo pia hawatasalimika,” kamanda mkuu wa bodi hiyo, Harun Ibn-Sina, amesema.

Harun pia alitoa wito kwa waislamu kuwasaidia mayatima na wahitaji katika kipindi cha mfungo kilichoanza Alhamisi.

Bodi hiyo ya Hisbah inatekeleza sheria za kiislamu huko Kano, ambapo jimbo hilo linatajwa kuwa na waislamu wengi.

Chanzo BBC

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags