Wastara: Ni ngumu kupata nafasi ya pili kwenye maisha

Wastara: Ni ngumu kupata nafasi ya pili kwenye maisha

Muigizaji mkongwe wa #BongoMovie Wastara Juma amewataka watu watumie vizuri nafasi na fursa wanazo zipata, huku akidai kuwa kwenye maisha ni ngumu sana kupata nafasi ya pili.

Kupitia ukurasa wake wa #Instagram msanii huyo ameandika

“Ukipata nafasi ya kuishi kwa furaha ishi furahia kama vile hautakufa milele, Ukipata nafasi ya ‘ukienjoy’ kula bata ponda starehe itumie vizuri sana kama vile duniani uko peke yako anaekula raha.

Na ukipata na nafasi ya kutubia kujutia na kuomba msamaha kuanzia kwa MUNGU mpaka kwa wanadaamu uliowakosea omba msamaha kama vile unakufa leo. Yote kwa yotee nafasi huwa hazijirudii ni mara chache sana kuipata nafasi kwa mara ya pili”.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags