Wasiojulikana wavamia chombo cha habari

Wasiojulikana wavamia chombo cha habari

Watu wasiojulikana wanaodaiwa kuwa majambazi wamevamia Television ya serikali nchini Ecuador siku ya jana Jumanne na kuwaweka chini ya ulinzi waandishi wa habari waliokuwa wakirusha kipindi moja kwa moja (live).

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa tukio hilo limetokea baada ya Rais kutoka nchini Ecuador Daniel Noboa kuweka mikakati na mipango ya kudhibiti magenge ya Mihadarati.

Watu hao ambao wameficha nyuso zao waliwashikiria mateka baadhi ya waandishi wa habari huku wakituma ujumbe kwa Rais Noboa kusitisha shambulio lililopangwa kudhibiti magenge hayo.

Mpaka kufikia sasa inaelezwa kuwa baadhi ya majambazi hao wameshatiwa nguvuni mwa polisi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post