Wasanii 45 wasiolipa fedha za mkopo kukiona

Wasanii 45 wasiolipa fedha za mkopo kukiona

Na Mintanga Hunda 

Kutokana na baadhi ya wasanii kutolipa madeni ya mikopo waliyopewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Hamisi Mwinjuma, amesema takribani wasanii 45 wanadaiwa hivyo wanatakiwa kulipa haraka iwezekanavyo kwa muda waliokubaliana.


“Mimi ni kiongozi lakini upande mwingine ni msanii hivyo nawajua wote kwa yeyote anayedaiwa ni lazima alipe kwani hakuna hata senti mia itakayobaki kwa mtu,” amesema Mwinjuma na kuongezea
“Baadhi ya wasanii wamechukua mkopo kwa makusudi hawataki kulipa hivyo watu wa aina hii wanatafuta ugomvi na mimi,” amesema.

Licha ya hayo ameahidi kukaa na viongozi wenzake, kujadili namna ya kupunguza baadhi ya masharti ili kurahisisha marejesho kwa wale wanaodaiwa.

Nyakalo Mahema ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa wasanii ameishukuru Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuongeza fedha kwenye mfuko huo kutoka Sh 1.6 bilioni hadi Sh 3 billioni kufikia mwaka huu.

“Kwa kiasi kilichoongezwa ni wazi kabisa wasanii wetu watapata mikopo ya kutosha kwani kiasi kilichopo ni kikubwa”, amesema Nyakalo

Mwigizaji Steven Jacob, akiwakilisha wasanii wengine nchini, amemtoa shaka Naibu Waziri kwa kudai kuwa madeni yote yatalipwa kwa njia yoyote.

“Tutakaa wenyewe kwa wenyewe kama wasanii na kusisitizana tulipe mikopo tunayodaiwa ili kuendeleza mfuko wetu,”amesema

Ikumbukwe kuwa awali wasanii hao walikuwa wakikopeshwa fedha zilivyokua zinashikiliwa na mfuko. Hivyo kutokana na usumbufu huo Wizara imeamua kuweka fedha benki hivyo msanii akitaka mkopo atamalizana na watu wa benki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags