Wapinzani wa Yanga wamtimua ‘Kocha’

Wapinzani wa Yanga wamtimua ‘Kocha’

Wapinzani wa Yanga SC hatua ya makundi CAF, CR Belouizdad ya Algeria wamemfukuza kazi  ‘kocha’ mkuu wa ‘timu’ hiyo Sven Vandenbroeck.

Taarifa ya ‘klabu’ hiyo iliyotoka leo Oktoba 8, 2023 imesema,  “Mwenyekiti wa Bodi ya ‘klabu’ ya CR Belouizdad, Mahdi Rabhi, amesitisha mkataba wa kocha wa Ubelgiji ‘Svan Vandenbroek’ kwa makubaliano ya pande zote na kumuondoa kwenye benchi la ufundi la ‘timu’ kutokana na tofauti ya kimtazamo kati ya pande zote.”

CR Belouizdad imepangwa kundi D kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Al Ahly ya Misri, Yanga SC ya Tanzania na Medeama ya Ghana.

Jana ikiwa nyumbani kwao, CR Belouizdad ilichapwa mabao 3-2 na USM Khenchela mchezo wa Ligi Kuu Algeria ikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ‘ligi’ hiyo ikiwa na alama tatu baada ya michezo miwili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags