Wanne wafariki katika shambulio, Marekani

Wanne wafariki katika shambulio, Marekani

Takriban watu wanne wameuawa huku watoto wawili wakijeruhiwa katika shambulio la risasi lililotokea jana Jumatatu Julai 03, 2023 katika mji wa Philadelphia nchini Marekani.

Kamishna wa Polisi wa Philadelphia, Danielle Outlaw amesema waliopoteza maisha wote ni wanaume wenye umri wa kati ya miaka 20 na 59 na watoto waliojeruhiwa wana miaka miwili na 13.

Amesema wamemkamata mtu mmoja mwenye umri wa miaka 40 anayesadikiwa kufanya tukio hilo. Mtuhumiwa huyo alikuwa amevaa nguo ya kuzuia risasi akiwa amejihami kwa bunduki karibu na eneo la tukio. Pia uchunguzi unaendelea kufanyika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags