Katibu mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa imewaasa wanawake mkoani Kilimanjaro kuachana na taasisi za mikopo maarufu kama ‘kausha damu’.
Ambapo hupata changamoto katika marejesho na badala yake wachukue mikopo ya halmashauri ambayo haina riba kabisa.
Katibu huyo amesema, “kuna hizi taasisi ambazo zimeanzishwa sasa hivi zinaitwa kaushadamu, si mnazijua? ni taasisi za kuangalia sana, kwasababu riba yake ni kubwa wewe kwasababu hujui, ukiomba leo utapata kesho na kweli unapata, lakini utakuja kulipa 100%”
Ameendelea, “utanyang’anywa kitanda, utanyang’anywa kila kitu na hapo utakuwa umerudi nyuma chukueni mikopo ya halmashauri ni mizuri kuliko mikopo mingine yeyote mikopo ambayo haina riba kabisa, ukichukua shilingi 1,000 utarudisha 1,000” alisema katinu huyo.
Leave a Reply