Wanaotumia Vision Pro wakati wa kuendesha gari watakiwa kuwa makini

Wanaotumia Vision Pro wakati wa kuendesha gari watakiwa kuwa makini

Baada ya kusambaa kwa video ikiwaonesha baadhi ya madereva wa #Tesla wakitumia kifaa cha ‘Vision Pro’ wakati wakiendesha magari, Katibu wa Uchukuzi Marekani Pete Buttigieg, atia neno.

Buttigieg, kupitia ukurasa wake wa X (zamani twitter) amewataka watumiaji wa vifaa hivyo kuongeza umakini ili kutohatarisha maisha ya wengine wakati wa kuendesha magari yao.

Vision Pro, ni kifaa ambacho kimezindulia na kampuni ya Apple kwa lengo la kuepusha kuwa na mzigo wa vitu vingi kwa wakati mmoja, chenye muundo wa miwani ambacho unaweza kukitumia kama simu, kompyuta, kuangalia movie na mambo mengine.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post