Wanandoa wauza mali zote, Wakaishi kwenye meli

Wanandoa wauza mali zote, Wakaishi kwenye meli

Wanandoa kutoka nchini Marekani wajulikanao kama John Hennessee, na mkewe Melody Hennessee wanadaiwa kuuza mali zao zote kwa ajili ya kwenda kuishi kwenye meli.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari kutoka nchini humo vimeripoti kuwa wanandoa hao walibainika kuwa mwaka 2020 waliuza nyumba pamoja na biashara walizokuwa wakiziendesha Florida na kununua gari maalumu lenye makazi ndani yake, ili waweze kusafiri sehemu mbalimbali nchini Marekani.

Aidha safari yao ya kuishi kwenye gari iligonga mwamba mpaka pale walipoona tangazo kupitia mtandao wa Facebook la kusafiri siku 274 ndani ya meli tangazo ambalo lilitolewa na kampuni ya ‘Royal Caribbean’ nayohusika na masuala ya meli.

Mpaka kufikia sasa John na Melody wameshatembelea mataifa mbalimbali yakiwemo Australia, New Zealand, Canada, Misri na Pasifiki ya Kusini, huku wakiweka wazi kuwa maisha ndani ya meli ni rahisi kuliko kuishi ardhini kutokana na kutodaiwa kodi yoyote.

Na sasa wawili hao wanafikiria kuchukua makazi ya kudumu katika meli ya kitalii ya ‘Villa Vie’ ambayo asilimia 30 ya wasafiri watapatiwa makazi ya kudumu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags