Wanajeshi kutoka nchini Sudani wamekimbia nchi yao kukwepa mapigano yanayoendelea na wamekimbilia nchi jirani ya Chad wakihofia kuuawa na wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces ‘RSF’ kinachopambana na wanajeshi wa baraza kuu la Sudan lililo chini ya Jenerali Abdel Fattaf al-Burhan
Aidha waziri wa ulinzi wa Chad, Jenerali Daoud Yaya Brahim amesema kuwa "wanajeshi hao waliwasili kwenye ardhi yetu wakipokonywa silaha na kuwekwa kizuizini siku ya Jumapili” alisema Jeneral Daoud
Jeneral huyo aliendelea kuzungumza licha ya vita inayotokea zaidi katika jiji la Khartoum kuwahusu wasudan wao kwa wao lakini wanachukua tahadhari dhidi ya mapigano hiyo ambayo yanadaiwa kusababisha vifo vya watu takribani 270.
Leave a Reply