Na Aisha Lungato
Niaje niaje! wasomi, niliwakumbuka sana sasa leo nimerudi tena ndugu yenu nisiye na hiyana kuja kuwapa nondo ambayo itaweza kuwasaidia huko mbeleni mnakoelekea, chakuzingatia ni kuwa bado hujachelewa muda bado upo.
Msikariri maisha kwa sababu kuanza chuo ni jambo jingine kusoma kufanya mitihani ni kipengele kingine na ku-graduate pia ni mtihani mwingine, nimeongea hivi kwa sababu kuna mambo mapya utajifunza kupitia hayo yote, jambo kuu ambalo naweza kukushauri leo ni kuwa taaluma unayosomea inamambo mawaili inaweza kukutoa kimaisha yaani ndiyo ikakupatia kipato vilevile pia ndiyo hiyo hiyo itakayo ‘kufelisha’.
Cha msingi ninachotaka kuzungumzia hapa ni kuachana na fikra hizo kuwa unachosomea kitakusaidia kufanikisha maisha yako, sikukatazi kusoma au kumaliza bali nakupa tahadhali kalba mambo mengine hayajakuelemea, najua wapo walikushauri usome faculty hiyo unayosomea kwa sababu ni rahisi kupata ajira nk.
Hata kama umeshauriwa hivyo basi usibweteke na ulichoambiwa, siku hizi bwana kama huna ndugu kwenye kitengo ambacho unataka kufanyia kazi basi kupata kwako kazi inakuwa mtihani sana na ndiyo maana wahitimu wengi wanaamua kujiongeza kwa kutafuta pesa kupitia vipaji walivyonavyo.
Vile vile kwako unatakiwa kujitazama kuanzia sasa hivi unakipaji gani, au kuna ufundi gani unaweza kuufanya nje ya masomo yako ambao utakuingizia kipato hii itakusaidia hata hapo baadaye mambo yatakapoenda kombo hiyo fani inaweza kukusaidia katika kuendesha maisha yako.
Ili kuonesha msisitizo katika hili tukaamua sisi kama @mwananchiscoop kutafuta mwandishi na mshauri katika nyanja mbalimbali aitwaye Jiwa Hassan ambaye hivi karibuni aliweza kupata umaarufu kupitia mitandao ya kijamii baada ya kufanya mahojiano yake na moja ya chombo cha habari nchini alipokuwa akieleza kuhusiana na ‘wanawake hawataki hela, wanataka muda wa wanaume’ ametoa ushauri kwa baadhi ya wanafunzi kwa kueleza.
“Vijana wa siku hizi huwa wanafurahia sana kuanza chuo kwa sababu jambo la kwanza anafikiria kuwa huru licha ya kuanza kujifikiria yeye mwenye na faculty aliyoichukua, so mimi sitaki kwenda mbali sana lakini ushauri wangu ni kujitahidi kuwatazama watu wao wa karibu ambao wameshamaliza vyuo na hawana ajira wataweza kugundua skills za maisha waache kubweteka na kufuata mikumbo” amesema Jiwa Hassan
Hatukuishia hapo katika pitapita zetu tukakutana na mwanafunzi ambaye ni muhitimu katika Chuo Cha Tumaini University (TUDACO) aitwaye Amiri Msuya aliyehitimu mwaka mmoja uliopita ambaye kwa sasa anajishughulisha na biashara ya nguo za kiume pamoja na kujitolea katika kitua cha redio akiwa kama Producer amefunguka na kueleza
“Zamani wakati niko chuo nilikuwa nikiambiwa kuhusu kutobweteka na ninachosomea niliona kama wanaoniambia maneno hayo wanaongopa lakini baada ya kurudi mtaani nimegundua kuwa sikuutendea haki wakati nilokuwa nauchezea kula bata, i wish nyakati zirudi nyuma but ndiyo haiwezekani” amesema Amiri
Aidha aliendelea kwa kutoa ushauri kwa wanafunzi ambao bado wako chuo kuanza kufikiria maisha yao ya mbeleni kabla ya kurudi mtaani huku akisisitiza kwa kusema kuwa mtaani ni kugumu na kupata ajira imekuwa changamoto sana.
I hope tumekuamsha kwenye usingizi ulilala kwa namna moja ama nyingine, cha kuzingatia zaidi ni kuachana na mikumbo ya marafiki ambao wanakushauri kula bata, pesa ya boom wakati unaweza kufungua biashara ambayo ikakupa maokoto ya maana, so amka bado haujachelewa ndiyo kwanza mwaka bado mbichi kabisa unaweza kufanya jambo.
Leave a Reply