Wanachuo  jifunzeni njia za kupata wazo la biashara

Wanachuo jifunzeni njia za kupata wazo la biashara

Na Michael Onesha

Pande za vyuo mambo vipi! leo tena kipande hiki cha uncorner tumewaletea makala inayohusu masuala ya biashara kwa wasomi wa vyuo, ili kuishi maisha yasiyoumizwa na ukata wa fedha.
Wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kulijenga liwe lenye tija kwako na kwa jamii nzima, pindi biashara inapoanza ili iwe na muendelezo mzuri kutokana na mahitaji ya jamii.

Hizi ni njia za kupata wazo la biashara
1. Tumia ujuzi ulionao
Ujuzi ulionao ndiyo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la biashara, Mfano kama wewe una ujuzi ama uliwahi fundishwa ufundi wa kushona nguo, why usianzishe biashara ya aina hiyo? Kama ulijifunza ufundi magari why usianzishe gereji yako? Ujuzi ulionao ndiyo hazina ya kwanza na ya kipekee ya kupata mafanikio, na utaweza kuifanya siku za weekend.

2. Badilisha hobby yako kuwa pesa
Hobby ni moja ya mambo ambayo watu hunufaika nayo, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga na kuuza mbwa? Kama Hobby yako ni kuogelea, kwa nini usianzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wanakuja huko kuogelea? Kama unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening.

3. Nunua biashara ambayo tiyari ipo
Ukishindwa kabisa kupata wazo unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuiendeleza, siku hizi kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua na kuendelea nayo, kwa mfano kukaribia Ramadhani unaweza kwenda Kariakoo kununua Abaya jumla nawe ukauza rejareja.

4. Tumia personality yako
Kuna mtu unakuta either ni mrembo sana, handsome , unaweza kutumia huo urembo kufanya biashara, either za marketing, branding ya biashara za makampuni makubwa pia kuna watu ni talkative sana so unaweza kutumia personality yako ukafungua biashara chuoni na ikawa kubwa ikatambulika sana.
5. Nini kinakosekana mtaani?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni chuoni kwako, kijijini kwenu au maeneo unayoenda kustarehe. Unaweza kujiuliza maswali machache tu ambayo yatakupa muongozo
-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, ndugu, majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

6. Tumia teknolojia kuanzisha biashara
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la biashara.
Mfano sasa ni kipindi cha joto, unaweza kwenda kuzungumza na wafanyabiashara wa viyoyozi ukawa unawatangazia bidhaa na wewe ukaweza kupata chochote kitu.

7. Copy business idea ambayo imefanikia nchi nyingine
Hii ni moja ya njia zinazotumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko ukaja kuifanyia kazi, kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika, mfano mzuri mikoba ya ‘Mama Africa’ kwa sasa imetapakaa duniani kote hii yote ni kutokana na watu kuchukua mawazo ya watu wengine na kuyaboresha, mfano siku hizi katika mikoba hiyo unaweza kuandikiwa hata jina lako hii yote ni ubunifu.



8. Tumia njia zote za kiutafiti kupata wazo la biashara
- Maonesho ya biashara
- Magazeti
- Kwenye taasisi za uma zinazohusika na biashara
- Kwa marafiki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags