Waliopinga utawala wa Mfalme Mswati wahukumiwa jela miaka 20

Waliopinga utawala wa Mfalme Mswati wahukumiwa jela miaka 20

Mahakama kutoka nchini Eswatini imewakuta wabunge wawili na hatia ya mauaji na ugaidi kwa jukumu lao katika wimbi la maandamano yaliyoikumba nchi hiyo mwaka 2021.

Mduduzi Bacede Mabuza na Mthandeni Dube, walizuiliwa baada ya kushiriki katika maandamano ya kuunga mkono demokrasia katika kile ambacho ni utawala wa mwisho kabisa wa kifalme barani Afrika. Jambo ambalo limepelekea kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

Hata hivyo, walikana mashtaka ya kuchochea machafuko. Huku Amnesty International ilisema hukumu hizo ni ushahidi wa kuendelea kuwakandamiza wapinzani.

Eswatini imekuwa ikiongozwa na Mfalme Mswati III tangu 1986 na vyama vya kisiasa vimepigwa marufuku kushiriki katika uchaguzi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags