Waliofutiwa matokeo ya kidato cha nne waruhusiwa kurudia mitihani

Waliofutiwa matokeo ya kidato cha nne waruhusiwa kurudia mitihani

Na Asha Charles

Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa idhini ya kurudia mtihani kwa wanafunzi 337 waliofutiwa matokeo yao ya  kidato cha nne kwa mwaka 2022 baada ya kuomba fursa ya kurudia mitihani huo.

Hii inaunganisha na wale wanafunzi 4 waliofutiwa matokeo na baraza la mitihani la taifa (NECTA) baada ya kuandika matusi kwenye mitihani yao.

Aidha waziri wa elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema utaratibu wa kurudia mitihani utakwenda sambamba na mitihani ya kidato cha sita ambayo inatarajiwa kuanza mei 2, 2023, na  watawekewa utaratibu wa kuchanganyika pamoja wakati wa kurudia mitihani hiyo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post