Walimu waruhusiwa kuingia na bunduki shuleni

Walimu waruhusiwa kuingia na bunduki shuleni

Wabunge wa jimbo la Tennessee nchini Marekani wamepitisha mswada wa kuwaruhusu walimu na wafanyikazi wengine wa shule kubeba bunduki shuleni siku ya Jumanne.

Imeelezwa kuwa wabunge hao ambao ni wanachama wa Republican wa Tennessee House walipitisha sheria hiyo kwa walimu na wafanyakazi wengine ambao walipata mafunzo ya kubeba bunduki ndani ya shule na maeneo ya vyuo vikuu.

Hiyo imekuja baada ya mwaka jana  kutokea shambulizi katika shule ya Kikristo ya Nashville lililosababisha vifo vya watoto watatu na watu wazima watatu.

Hata hivyo uamuzi huo unapingwa na Democrats, wanafunzi na watetezi mbalimbali ikiwa ni mwaka mmoja tangu mtu kufyatua risasi na kuwaua watu sita katika shule hiyo.

Sheria hiyo sasa imetumwa kwa Gavana wa Tennessee Bill Lee, ambaye hajawahi kupinga sheria yoyote katika nafasi yake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags