Walimu waondoa vioo vya chooni, baada ya wanafunzi kujirekodi

Walimu waondoa vioo vya chooni, baada ya wanafunzi kujirekodi

Shule ya Southern Alamance iliyopo Carolina nchini Marekani, imelazimika kuondoa vioo vyote katika vyoo vya wanafunzi kwa lengo la kuwazuia ku-rekodi video za TikTok muda wa darasani.

Uamuzi huo ulikuja baada ya kuona wanafunzi wakitoka darasani mara kwa mara ili kutengeneza maudhui ya TikTok, huku wakidaiwa kutoka darasani hadi mara tisa kwa siku.

Mbali na kuondoa vioo, shule hiyo iliamua kuweka CCTV camera katika kodro zote za shule hiyo ili kufuatilia miendendo ya wanafunzi wanaofanya usumbufu wakati wa masomo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags