Wakali wa kutupia ligi kuu bara

Wakali wa kutupia ligi kuu bara

Baadhi ya mastaa wa soka wanapenda maisha ya bata nje ya uwanja, kununua ndinga kali, nyumba, na mambo mengine pia wapo wanaopenda kuvaa na kupendeza. Hawa hapa mastaa kumi wa Ligi Kuu Bara wanaotupia asikuambie mtu.

1 Khalid Aucho (Yanga)

Jamaa anajua kutupia viwalo anapenda t-shirt na jeans huku chini akitupia raba kali. Kwenye rangi, ndiyo mwenyewe, havai pamba zenye rangi zilizochoka au kupoa, bila kusahau miwani myeusi.

2, Djigui Diarra (Yanga)

Kwenye maduka makubwa ya pamba humkosi anapenda kuvaa na hupendelea zaidi nguo za asili za nchini kwao. Kwenye suti, ndiyo kabisa, anajua kupangilia. Miwani ni kitu kingine ambacho huwezi kukikosa.

3 Clatous Chama (Simba)

Chama na kaptula hawaachani. Ingawa pia anaonekana sana akiwa amevalia jeans na t-shirt, lakini kaptula ina nafasi yake na siku zake raba nazo ndiyo usiseme.

4 Kennedy Musonda (Yanga)

Yeye hachagui chochote twende tu mavazi yanaukubali mwili wake na aina yoyote atakayovalia anapendeza yakinakshiwa na miwani au kofia na wakati mwingine hubeba kibegi huku chini akiwa na raba kali.

5 David Kameta ‘Duchu’ (Simba)

 

Kama ni kuvaa tu, Duchu anajua aisee. Mwili wake unakubali kila nguo na anapendelea sana kuvaa raba zenye soli kubwa na zinavutia. Suruali anazopendelea ni pana bila ya kusahau t-shirt kali na kwa mwonekano tu ni za bei kubwa.

6 Feisal Salum (Azam)

Anavaa mavazi yoyote na anatokelezea. Hata kanzu akivaa anapendeza ingawa mara nyingi anapendelea kuvaa viatu vya wazi na suruali kubwa na 'tisheti'. Pia raba na kofia zinamtoa.

7 Habibu Kyombo

Sasa ukute ametupia t-shirt, jeans na raba zake zile, utapenda.

Kuna wakati anavalia suti hasa kwenye baadhi ya mitoko na alikuwa kwenye vazi hilo ‘Kaunda suti’.

8 Dickson Job (Yanga)

Anajua kutupia sana na ukimkuta kwenye mitoko yake nguo alizovaa zinamfiti kwa kiasi kikibwa na havai mavazi makubwa. Anapendelea kuvaa 'tisheti', suruali, kaptura na raba kali.

 9 Kibwana Shomari

Mara kadhaa amekuwa akivalia suti, t-shirt, jeans, raba ingawa kwenye suti anapendeza kinoma, anapendelea pia kuvaa kaptura.

10 Kibabage (Yanga)

Nje ya uwanja, anapenda kuvalia t-shirt, jeans, kaptura na anamiliki raba nyingi kali hadi hajui avae zipi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags