Mahakama kutoka nchini Iran ilitangaza hukumu ya kunyongwa dhidi ya wanaume wawili siku ya Jumatatu ambao walihukumiwa kifo kwa kuukashifu uislamu, watuhumiwa hao walitambulika kama Yousef Mehrad na Sadrollah Fazeli Zare.
Aidha makosa hayo ya uhalifu yanajumuisha kukashifu Uislamu na Mtume Muhammad, na kwamba walitumia mitandao yao ya kijamii kusambaza chuki dhidi ya uislamu na kuhamasisha kutomuabudu Mungu.
Pamoja na Mahmoud Amiry Moghaddam, ambaye anaongoza shirika la haki za binadamu lenye makao yake Norway , Iran Human Rights, alisema katika taarifa, “ mamlaka kwa mara nyingine zimedhihirisha tabia yao ya kinyama kwa kuwaua watu wawili kwa kutoa maoni yao.”alisema Mahmoud
Huku ikitoa rai kwa jumuia ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti mara moja.
Leave a Reply