Wahamiaji wafukuzwa, Tunisia

Wahamiaji wafukuzwa, Tunisia

Mamia ya wahamiaji kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara (Afrika) wameshambuliwa katika mji wa Sfax nchini Tunisia huku zaidi ya watu 10 wakiripotiwa kujeruhiwa wakiwemo watoto.

Machafuko hayo ni ya kulipiza kisasi yakichochewa na mauaji ya raia mmoja nchini humo yaliyotokea wakati wa makubiliano dhidi ya wahamiaji Julai 3 mwaka huu.

Inadaiwa kuwa baadhi ya wahamiaji wameshambuliwa kwa Mapanga na kulazimika kuukimbia mji huo unaotumiwa na watu wanaotaka kuingia Ulaya kupitia kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags