Wafuasi wamiminika kwenye akaunti ya Yamal

Wafuasi wamiminika kwenye akaunti ya Yamal

Kiungo wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, Lamine Yamal ambaye hivi karibuni ametikisa vichwa vya habari baada ya kuwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Michuano ya Euro 2024, huku akiweka rekodi ya mchezaji kijana zaidi kufunga bao katika mashindano hayo alipofunga hatua ya nusu fainali dhidi ya Ufaransa, ameendelea kujizolea wafuasi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Katika kipindi cha siku 30 zilizopita, idadi ya wafuasi wa Instagram wa Yamal imeongezeka zaidi ya mara mbili, ikipanda kutoka wafuasi milioni 7 hadi milioni 17.

Utakumbuka kuwa alipofunga bao katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Ufaransa alikuwa na miaka 16 na siku 362, akiipiku rekodi ya Johan Vonlanthen aliyefunga katika michuano hiyo mwaka 2004 akiwa na miaka 18 na siku 141.

Pia Yamal bao lake hilo limeweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika michuano ya timu za taifa kwa wakubwa akiipiku ile ya Pele alipofanya hivyo akiwa na miaka 17 na siku 239 kwenye michuano ya Kombe la Dunia 1958.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags