Wafanyakazi wote Ugiriki wagoma kufuatia ajali ya treni

Wafanyakazi wote Ugiriki wagoma kufuatia ajali ya treni

Wafanyakazi  mbalimbali watashiriki katika mgomo wa nchi nzima nchini Ugiriki leo wakiandamana dhidi ya mkasa wa ajali ya treni ambao haukuwahi kutokea nchini humo na kufuatia watu 57 kufariki duniani, hata hivyo Kunatarajiwa kuwa na maandamano makubwa pia nje ya bunge huko Athens.

Mgomo huu utakaowajumuisha wafanyakazi mbalimbali kutoka sekta ya umma, unatarajiwa kukatiza katika usafiri wa mabasi, treni na hata feri ambazo zitakuwa zimetia nanga bandarini kwani mabaharia nao watajiunga na maandamano hayo.

Aidha tangu Alhamis iliyopita wafanyakazi wa reli nchini humo wamegoma wakidai kwamba madai yao ya mazingira ya usalama hayajatiliwa maanani kwa miaka sasa.

Chanzo DW


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post