Wafanyakazi PURA waaswa kuongeza juhudi kwenye utendaji

Wafanyakazi PURA waaswa kuongeza juhudi kwenye utendaji

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wameaswa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na uadilifu ili kuiletea tija sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka hiyo Charles Sangweni wakati wa kikao cha nne cha baraza hilo kilichofanyika hivi karibuni mkoani Morogoro.

“Tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha shughuli za mkondo wa juu wa petroli zinaleta chachu ya maendeleo kwenye mnyororo mzima wa mafuta na gesi asili nchini, na utendaji wetu kama wafanyakazi ndio utafanikisha hili,” alieleza.

Mhandishi Sangweni aliongeza kuwa ni vyema wafanyakazi wote wakajituma katika kutimiza majukumu yao ya kila siku huku wakiongeza ubunifu ili kuongezea thamani katika kile wanachozalisha.

Baraza hilo limeipitia na kujadili taarifa ya mapendekezo ya kuhamisha fedha kwa mwaka wa fedha 2021/22 pamoja na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23 kutoka idara na vitengo vya taasisi.

Aidha, baraza limejadili taarifa ya maoteo ya mapato ya taasisi kwa mwaka wa fedha 2022/23, hoja za wafanyakazi na masuala mengineyo yahusuyo utendaji kazi na hali bora kwa wafanyakazi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post