Wachezaji Yanga wapewa zawadi milioni 700

Wachezaji Yanga wapewa zawadi milioni 700

Wakati ‘Klabu’ ya Simba ikisitisha mkataba wake na aliyekuwa ‘kocha’ mkuu Robertinho, Uongozi wa ‘Klabu’ ya Yanga baada ya kufurahishwa na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Simba umeamua kuwapa wachezaji na ‘benchi’ la ufundi tsh 700 milioni kama zawadi.

Ambapo imeelezwa kuwa mapema kabla ya mchezo huo viongozi waliahidi kununua kila bao litakalofungwa kwa tsh 100 milioni, lakini kutokana na mzuka vigogo hao wakiongozwa na mfadhili wao GSM wameongeza mzigo na kufikia tsh 700 milioni.

Kwa mujibu wa Mwanaspoti wameeleza kuwa pesa hizo zikigawanywa kwa kila mchezaji na ‘benchi’ la ufundi huendea kila mmoja akaondoka na Sh 15 milioni.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho wachezaji wa Yanga kupata ‘bonasi’ kubwa ni miaka mitano iliyopia ambapo walipewa Sh 400 milioni walipoifunga Simba, bao lililofungwa na Zawadi Mauya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post