Wachezaji wa Man United wanadai ‘jezi’ zinawabana

Wachezaji wa Man United wanadai ‘jezi’ zinawabana

Inadaiwa kuwa wachezaji wa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited, wanalazimika kuvaa ‘jezi’ zisizo rasmi wakati wa ‘mechi’ kutokana na ‘jezi’ zilizotengenezwa na #Adidas, kuwabana sana.

Kufuatia malalamiko hayo, kampuni ya Adidas imeanza kutafuta suluhu ya haraka baada ya baadhi ya wachezaji kuacha kuvaa ‘soksi’ rasmi tangu mchezo wa pili wa msimu huu, dhidi ya Tottenham wakilalamika kuwa zilikuwa zikiwabana sana maeneo ya nyuma ya miguu (Vigimbi).

‘Golikipa’ wa ‘timu’ hiyo, #AndreOnana, aliacha kuvaa ‘jezi’ hizo rasmi kwa ajili ya wachezaji na kuhamia kwenye jezi zilizotengenezwa kwa ajili ya mashabiki, kuanzia kwenye ‘mechi’ dhidi ya #SheffieldUnited, Oktoba 2 mwaka huu.

Hata hivyo inadaiwa kuwa baadhi ya wachezaji wamelazimika kukata matobo nyuma ya ‘soksi’ zao kama suluhisho la muda, lakini inaonekana kuwa hivi sasa wameanza kuvaa soksi zilizotengenezwa kwa ajili ya mashabiki.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags