Wachezaji ndiyo wamezomewa Bandarini Dar es salaam

Wachezaji ndiyo wamezomewa Bandarini Dar es salaam

Zikiwa zimesalia siku nne kabla ya kufanyika kwa pambano la Dabi ya Kariakoo, leo kikosi cha Simba kimeanza safari kwenda Zanzibar huku kikizomewa na mashabiki wa Yanga.

Baada ya kuwasili bandari ya Dar es Salaam, mashabiki hao na watu wengine waliokuwepo eneo hilo, walianza kuwazomea wachezaji wakati wanaingia eneo hilo.

Simba imeondoka na wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza, akiwemo kipa chaguo la kwanza kwa sasa, Ayoub Lakred  aliyekosekana katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu uliopigwa Singida.

Watani hao wa jadi watakutana Jumamosi ikiwa ni mechi muhimu ambayo ina nafasi kubwa kwa timu hizo katika vita ya kuwania ubingwa wa ligi.

Yanga inaongoza msimamo ikiwa na pointi 55 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 46.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags