Waamuzi wa simba na Yanga wajulikana

Waamuzi wa simba na Yanga wajulikana

Muamuzi #AbongileTom kutoka nchini Afrika Kusini ameteuliwa kusimamia mchezo wa robo fainali ya ‘ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC dhidi ya #AlAhly kutoka nchini Misri.

Tom mwenye umri wa miaka 32 atakuwa katikati ya uwanja siku ya Ijumaa Machi 29 kwenye mchezo huo wa mkondo wa robo fainali ambao utachezwa saa 3:00 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Pia shirikisho la soka Afrika (CAF) limemteua muamuzi, Bamlak Tessema Wayesa raia wa Ethiopia kusimamia mchezo wa robo fainali ya ‘ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans SC dhidi ya #MamelodiSundown ya Afrika Kusini.

Mchezo huo utapigwa katika uwanja Benjamini Mkapa siku ya Jumamosi Machi 30 saa 3:00 baada Simba kukiwasha na Al Ahly.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags