Waachiwa huru kupunguza msongamano gerezani

Waachiwa huru kupunguza msongamano gerezani

Wafungwa 4068 walioshindwa kulipa faini mbalimbali wameachiwa huru nchini #Nigeria katika mpango wa kupunguza msongamano wa wafungwa Magerezani nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Olubunmi Tunji-Ojo amesema kumekuwa na changamoto katika kuwahudumia wafungwa ambao jumla yao kabla ya msamaha huo ni 80,804 katika Magereza 253.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) ya hivi karibuni inaonesha Nigeria inawafungwa na mahabusu mara mbili ya uwezo wa Magereza yaliyopo huku watuhumiwa wengi wakiwekwa ndani miaka kadhaa kusubiri hukumu zao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post