Mfanyabiashara kutoka Shinyanga, Sayida Masanja, amefungua kesi ya madai dhidi ya mtandao wa mawasiliano (Vodacom) kwa tuhuma za kushindwa kulinda, kuwezesha, kuruhusu na kutoa taarifa zake binafsi kwa mfumo wa akili bandia ya Chat GPT bila ridhaa yake.
Taarifa hizo ni pamoja na Simu zinazoingia na kutoka, IMEI, IMSI, utambulisho wake wa laini ya simu na taarifa zinazotambulika kibinafsi (PIIs).
Ingawa mtandao huo umekana kuhusika na tuhuma hizo na kuiomba Mahakama kuifuta kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa tena Sept. 13, mwaka huu.
Ikumbukwe sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi imeanza kutumika Tanzania tangu Mei 1, 2023, hivyo Mwananchi ana haki na wajibu wa kufahamu taarifa zako zinapaswa kulindwa kisheria na mkusanyaji, mchakataji au mtunzaji yeyote anayezifikia.
Leave a Reply