Viumbe wazuri zaidi duniani wenye ulemavu wa ngozi

Viumbe wazuri zaidi duniani wenye ulemavu wa ngozi

Duniani kuna mengi ya kustaajabu na kufurahisha, ukizungumzia vitu asilia basi suala kama hili huwezi kuacha kuligusia kuhusiana na viumbe wenye ulemavu wa ngozi.

Ukiangalia bila ya kusita unaweza dhani viumbe hao wameundwa kwa ajili ya filamu ya #Desney, wana manyoya meupe, halkadharika ngozi nyeupe, duh! Sikujua kama kuna nyoka weupe duniani.

Hali ya viumbe hao kuzaliwa na ulemavu wa ngozi ni nadra sana, ukizingatia watu wengi wamezoe kuona binadamu tu ndiyo huwa katika hali hiyo. Sasa tuangalie viumbe wazuri zaidi duniani wenye ulemavu wa ngozi.

  1. Farasi

Farasi wenye ulemavu wa ngozi ni wale ambao wana ngozi, manyoya na mkia mweupe, mara nyingi hawachanganyiki na wale wenye rangi ambazo watu wengi wamezizoea. Inaelezwa kuwa ulemavu wa ngozi kwa farasi hupatikana kwa kurithi kutoka vizazi kwa vizazi.

  1. Simba

Ni ajabu kuona #Simba weupe kwa sababu wengi wetu hatujazoea kuona simba wenye rangi hiyo, Kwa Afrika simba wenye rangi nyeupe kwa mara ya kwanza waliripotiwa kuonekana mwaka 1938 eneo la Timbavat nchini Afrika Kusini.

  1. Sokwe

Sokwe wa kwanza mwenye ulemavu wa ngozi alizaliwa Equatorial Guinea, mwaka 1966, alichukuliwa na  kupelekwa kwenye Bustani ya Wanyama ya Barcelona nchini Uhispania, ambapo aliishi hadi kifo chake kutokana na saratani ya ngozi mwaka 2003.

  1. Nyoka

Nyoka wenye ulemavu wa ngozi ni aina ya nyoka wanaokuwa na tatizo la kimaumbile la ukosefu wa rangi mwilini na machoni, tatizo hilo pia husababisha macho ya nyoka hao kuwa na rangi nyekundu, mara nyingi wanakuwa na uwezo mdogo wa kuona.

  1. Mbwa

Mbwa wenye ulemavu wa ngozi wanaojulikana kama Doberman weupe huzaliwa na kutambulika kuwa na ulemavu huo kutokana na ngozi zao kuwa na rangi ya ‘krimu’, na sio weupe kabisa.

  1. Kasa

Kasa wenye ulemavu ni nadra kuonekana wapo wachache sana, utofauti wao huonekana kwenye gamba la juu ambalo huwa na rangi tofauti, wataalamu wengi husema kuwa ni rangi ya pink.kwa upande wa kasa wao hupata ulemaavu huo kutokana genes zikigongana.

  1. Tausi

Ukizungumza ndege warembo zaidi duniani huwezi acha kumtaja #Tausi kwa sababu ya urembo wake unao wavutia wengi. Wapo #Tausi wenye ulemavu wa ngozi ambao huwa na manyoya meupe yenye kupendeza.

Tuambie kiumbe yupi amekuvutia zaidi?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags