Vitu vya kula kabla na baada ya mazoezi

Vitu vya kula kabla na baada ya mazoezi

Habari msomaji wa magazine yetu ya MwananchiScoop natumaini u mzima wa afya tele na unaendelea vema kabisa na majukumu yako ya hapa na pale.

Leo basi katika dondoo za fitness tumekusogezea vitu vya kula kabla na baada ya kufanya mazoezi.

Najua wanafunzi wengi sasa hivi mnapenda kufanya mazoezi lakini wengi wao hamtambui ni vitu gani unapaswa kula kabla na baada ya mazoezi hayo, kutaka kujua ungana nami leo.

Tunajua kuwa licha ya mazoezi unayofanya kila siku ni muhimu sana kufahamu vitu vya kula kabla na baada ya mazoezi hayo, maana vyakula hivyo vina mchango muhimu kwa afya yako.

Kwa ajili ya kufurahia na kupata faida ya mazoezi hayo ambayo mara nyingi huchukua nguvu nyingi ya mwili ni vizuri kuwa mwangalifu ni kiasi gani cha chakula utatumia.

Hakikisha kabla ya mazoezi yoyote unapata kiasi kidogo cha chakula kitakachokufanya uwe na nguvu wakati wa mazoezi ili kuimarisha nguvu ya misuli yako ili uweze kuchoma kalori nyingi na kuboresha afya ya mwili wako bila tabu yoyote.

Hakikisha unakula saa 1-2 kabla ya mazoezi na kisiwe na kalori zaidi ya 300-500 usile chakula mara na kuanza mazoezi.

Unaweza ukala ndizi au mkate wa ata (brown bread), oatmeal au viazi vikuu vichache.

 

Baada ya mazoezi hakikisha unakula baada ya dakika 20-60 ili mwili wako uweze kurudisha virutubisho vilivyotoka wakati wa mazoezi, hakikisha unachanganya vyakula vya wanga vyenye afya na protini vyenye kalori 400.

Vyakula hivyo ni kama:-

Kuku na wali wa kahawia au (Brown rice), yai na mkate uliochomwa vizuri, lozi na maziwa mgando au chokoleti zisizo na sukari kwa wingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post