Vita yasababisha tamasha la Bruno kufutwa

Vita yasababisha tamasha la Bruno kufutwa

Tamasha la mwanamuziki kutoka nchini Marekani #BrunoMars lililopangwa kufanyika Tel Aviv, Israel usiku wa Jumamosi ya wiki iliyopita limefutwa baada ya vita kuibuka nchini humo.

Tamasha hilo ambalo ilikuwa ni la pili kwa Bruno kulifanya nchini humo baada ya lile la kwanza  kufanyika siku ya Jumatano, ilikuwa imepangwa kuhudhuriwa na zaidi ya mashabiki 60,000.

Kitendo cha kughairishwa kwa tamasha hilo kimewanyima waandaji na waratibu wa kampuni ya Live Nation Israel zaidi ya tsh 75 bilioni  ambazo walizikusanya kwenye mauzo ya ‘tiketi’.

Kwa mujibu wa ‘ripoti’ kutoka Business Insider tayari ‘tiketi’ zote ziliuzwa na kilichokuwa kinasubiriwa ni show tu kufanyika lakini baada ya machafuko kutokea tamasha hilo lilifutwa.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali ni kwamba ‘show’ hiyo ilikuwa inagharimu Dola 500 kwa kiingilio cha chini.

.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags