Licha ya muziki kuhusisha usikilizaji zaidi lakini video zake zimekuwa na mchango mkubwa wa kukuza kazi za wasanii na kuwapeleka mbali zaidi. Pia zinapanua wigo wa sanaa na kutoa ajira kwa watu mbalimbali kama vile waongozaji wa video, wabunifu wa mavazi, wapiga picha na hata watu wa make-up
Mara zote Video huzifanya nyimbo kuwa na uhalisia na kilicho imbwa ndani. Msikilizaji anaposikia wimbo na kutazama video ambayo inauhalisia na kile kilichoimbwa huongeza mashiko zaidi.
Muda mwingine anaweza kuhisi kaimbiwa yeye kutokana na kile kilichowasilishwa mfano wa nyimbo kama Nitarejea ya kwake Diamond ft Hawa, dhima ya waandishi hao kuhusu walichoimba ndani ni kuonesha Umasikini, Mapenzi na Kujali. kwenye Video yake pia walifanikiwa kuonesha vitu vyote hivyo.
Aidha husaidia kuinua nyimbo tena na kuvuma zaidi, shabiki anaweza kupenda wimbo kutokana na video yake ilivyorekodiwa na ubora wake.
Wengi wao baada ya kutazama video hujikuta wakipenda hadi mashairi yake. Mara nyingi hii imekuwa ikitokea kwa wasanii wengi hata hapa nchini.
Sambamba na hayo video kwenye kuvumisha nyimbo pia huwapa wasanii mafao makubwa mfano kupitia majukwaa ya kutazamia video za muziki kama YouTube msanii anaweza kupata faida na hii ni sehemu nyingine ambayo wasanii hupiga hela.
Nini kinahitajika kwa wasanii ili kuzalisha video kali zaidi?
Jukumu la kupata kitu kizuri kwenye video sio tu la muongozaji lakini pia msanii na timu yake, wanahitajika kuchukua nafasi kubwa ili kufanikisha japo.
Ubunifu hatuwezi kuupata kwa kila mtu lakini kama msanii inabidi usiishie tu kuimba mashairi mazuri lakini pia hata kuonesha uwezo wako kwenye video.
Ikitokea unaigiza kwenye video hiyo kama muigizaji mkuu, ukiachana na kuimba basi inabidi ufanye kwa ubora mkubwa. Hapa sasa ndio utaona uwezo wa msanii kwenye kufanya vitu vingine.
Msanii anatakiwa pia kushiriki kwenye uzalishaji wa video husika. Msanii anatakiwa kutoa mawazo yake kuhusu video, nini kiwepo au nini kisiwepo na kipi kiongezwe lakini pia wape nafasi wengine kuwasikiliza na usiwe msemaji wa mwisho.
Leave a Reply