Verrtti kutua Man United

Verrtti kutua Man United

Licha ya kudaiwa kuwa ‘mabosi’ wa #Al-Hilal kufika #Ufaransa kwa ajili kumuwinda kiungo wa #PSG, #MarcoVerrtti, lakini hawajafikia ‘klabu’ ya #ManchesterUnited yenye shauku na dhamira kubwa ya kumchukua mchezaji huyo.

Aidha Man United imeonyesha nia ya kutaka kumsajili fundi huyu kwa sababu Fred ameondoka, huku kukiwa hakuna uhakika wa kuendelea kusalia na kiungo wao mwingine Scott McTominay, hivyo eneo lao la kiungo lina upungufu mkubwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya L’Equipe inaeleza pamoja na mazungumzo ya wawakilishi wa kiungo huyu na Al-Hilal bado kuna uwezekano mkubwa akatua Man United ikiwa watafikia makubaliano na mabosi wa PSG.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags