Vazi la kaunda suti linavyo waka mjini

Vazi la kaunda suti linavyo waka mjini

Niaje!! Ni weekend nyingine tunakutana tena watu wangu wa faida mimi najuaga mko vyema kabisa basi sina budi kusema kazi iendelee kwa mujibu wa mama Samia, lengo na nia ni yaleyale tu kuelekezana na kujuzana mambo mbalimbali katika kipengele chetu cha fashion.

Leo katika fashion tumekusogezea namna ambavyo vazi la Kaunda suti linavyo waka na kuwavutia watu wengi hususani vijana katika kipindi cha hivi karibuni limechukua umaarufu sana.

Ebwana imekaa hivi katika vazi la Kaunda suti limetokana na suti imeonekana nivazi linalo mpendeza kila mtu na kumheshimisha mtu yeyote anapo vaa kuanzia waheshimiwa hadi wana mitaani.

Hata mtu akitaka kwenda siku ya kwanza kujitambulisha ukweni ni vazi mmoja wapo litakufanya uonekane smart mbele ya wakwe bana hahahaha, nakupa chukua hiyooo.

Hii aina ya Kaunda suti  hivi ulishawahi jiuliza ilianzia wapi sasa hata usijali team Scoop itaweka bayana, vazi la Raisi wa zamani kutokea nchini Zambia Mh. Kenneth Kaunda alionekana akivyalia suti za mtindo wakwake peke ake kiasi cha kupachikwa jina Kaunda suti kwa wale ambao mlikuwa haujui.

Vazi hili ndio lilikuwa la mzee Kaunda mwenyewe ambae kwasasa hatuko nae tena duniani ila ametuachia mtindo wa Kaunda suti tuna tambaa nao wana fashion najua watoto wa elfu mbili tumewaacha hapo.

Kaunda suti kwa bongo land yetu hapa imepata umaarufu sana kwasababu inavaliwa na kila rika mbalimbali kiasi cha kuonekana ni vazi ambalo ni smple and smart kwa kila mtu.

Ila kwa upande mwengine vazi hili miaka ya 1920 wafaransa wawili Ted Lapidus na Yves Saint Laurent walikuwa wabunifu wa mitindo waliweza kubuni vazi la Kaunda suti ilikuwa likiitwa “safari suti”lengo lilikuwa kubuni suti simple za kusafiria.

Sasa team ya Mwananchi Scoop ikasogea moja kwa moja mpaka Tandika kwa mshonaji na mwanamitindo wa kaunda suti za kike na kiume bwana Zuberi Suleiman yeye ameanza kushona kaunda suti za watu wajinsia hizo mbili tokea mwaka 2010, punde tu alipo maliza elimu yake ya juu akaona bora aingie kwenye mitindo na fashion anasema.

“Nilivutiwa sana na mitindo hasa mitindo ya kushona suti ila ilikuwa ngumu sana nyumbani kuacha taaluma nilio somea wazazi hawakuni elewa ila naifurahia kazi yangu”alisema Zuberi.

Zuberi anasema kazi yake ina mpatia kipato cha kujikimu na maisha yake alizungumzia biashara yake wateja anao kuja kununua na kushona Kaunda suti ni wengi kuliko matarajio yake amesema.

“Saivi vazi la Kaunda suti kwanza limekuwa vazi ambalo unaweza kuvaa hata kwenye masherehe, so wateja wangu wengi ni watu wanao udhuria sherehe au mikutano mbalimbali”alisema kijana huyo.

Kwa upande wa bei yeye kwake hakuna shida huwa ana angalia na mfuko wa mteja ndipo wanapataja bei “the way utakavyo mteja tu ila kianzio nauza Kaunda kuanzi elfu 40 nakuendelea na hakuna mteja aliekuja kwangu akawa na dout juu ya bei kwasababu huwa najaribu kumpa mteja ufafanuzi kabla sijaa andaa nguo yake” alisema mwanamitindo huyo.

Aliendelea kusema wateja wake huwa wanamfata ofisini kwake kutokana na umaarufu wake eneo hilo japo kwenye mitandao ya kijamii anaitangaza biashara yake lakini ni mara chache sana kupata wateja kwanjia ya mitandao.

Aidha changamoto anayopitia katika biashara yake pale anapokuwa na wateja wengi bidhaa zinakua chache anasema “chungu katika biashara yangu unakuta mzigo wa kaunda ukiisha natakiwa nikafate vitambaa vyengine niweze kushona sasa sometimes inanipa wakati mgumu ninapoenda kuchukua vitambaa nikakosa rangi alio taka mteja” alisema Zuberi.

Haya ndio mambo ya fashion angalia kila fashion isikupite mjini mtu wangu sisi kwenye kipengele hiki kwa wiki tunashusha kalamu chini  wazungu wanasema til next time.

 

    

 

  

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags