Vazi la heshima alilovaa mke wa Kanye West lageuka gumzo

Vazi la heshima alilovaa mke wa Kanye West lageuka gumzo

Mke wa mwanamuziki kutoka Marekani #KanyeWest #BiancaSensori amewashangaza wengi baada ya kuvaa vazi la heshima akiwa matembezi na mumewe nchini Japan.

Vazi alilovaa Bianca ndiyo limewashangaza wengi kwani alizoeleka kuvaa nguo za nusu utupu kila anapokuwa matembezi na mumewe.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 ameonekana akiwa amevalia gauni la ‘Beige flowy maxi’, huku akitupia na kitambaa cheusi kichwani naye mumewe Kanye akivalia vazi jeupe.

Wawili hao wamewasili siku Jumamosi katika nchi hiyo kwa ajili ya mapumziko ikiwa ni siku chache baada ya kuonekana nchini Italia kama ilivyo kawaida yao.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni marafiki wa Bianca walidai Kanye anamchukulia mkwewe kama mradi wa sanaa kwa kumvalisha mavazi yanayoonesha nusu ya mwili wake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post