Uvaaji  wa vipini na hereni kwa wanaume

Uvaaji wa vipini na hereni kwa wanaume

Leo katika Fashion mambo yamekuwa mengi na this time nita-deal na fashion kwa wanaume jinsi gani wanavyoonekana katika urembo wa hereni na vipini.
Yaweza kuwa niajabu kwa wazee wetu wa karne za nyuma lakini ndiyo hivyo mambo ya fashion bana na kwenda na wakati kutokana na utandawazi unavyotaka katika Fashion, siku hizi kumekuwa na fashion mbalimbali ambazo zamani zilikuwa azifatiliwi kabisa au ulikuwa unaziona kwa watu wachache.

Miaka ya nyuma ilizoeleka wanawake pekee ndiyo wanastaili kuvaa hereni na vipini puani na hata wengine kutoboa kabisa pua na kuweka vipini na wengi wao walipendelea zaidi kuvaa upande mmoja wa pua na mwingine kubakia kawaida.

Lakini siku hizi imekua tofauti kidogo Tanzania wanaume pia wameanza kutumia urembo huu wa hereni na vipini puani na imeonekana kuwapendeza vilevile.

Urembo huu umeanza muda kidogo na ulivaliwa sana na wanawake wa pwani na mara nyingi tulizoea kuwaona wa dini ya kislaam haswa wakipendeza na mtindo huu wa vipini, siku hizi imekua tofauti kidogo haswa miaka ya hivi karibuni ‘staili’ hii imerudi kwa kasi zaidi na ubora wa hali ya juu.

Siyo watu wa pwani tu wanaotumia urembo huu hata wengine pia vilevile siyo lazima kutoboa pua na kuvaa upande mmoja wa pua. ‘staili’ imekuja kivingine zaidi waweza vaa katikati ya pua kama picha zinavyoonesha haswa wanawake au kutoboa kabisa pua na kuweka kipini sehemu zote mbili za pua.


Lakini wengi hupendelea moja na kwa upande wa wanaume ni muhimu kutoboa kabisa ili kuweka muonekano mzuri na wakuvutia waweza fanya hivyo kwa pande zote mbili za pua au upande mmoja na kufanya muonekano wako kuwa tofauti zaidi.
Tukumbuke ni asilimia ndogo sana ya watu wanaokubaliana na muonekano huu Afrika haswa hapa nchini kwetu Tanzania na vilevile inakua ngumu zaidi kwa upande wa jinsia ya kiume, tuwe makini katika hili japo urembo huu ni kama urembo mwingine na umeanza tangu enzi za mababu zetu.

Mwananchi Scoop kama kawaida hatupitwi na jambo moja kwa moja Sharifu Hamadi yeye ni mfanyabiashara wa Kariakoo kazi yake kubwa ni kuuza vipini vya puani, hereni na urembo mwingine, anaeleza kuwa siku hizi soko lake limebadilika sana kutokana na wateja wake kuwa wa kiume ingawa na wanawake huwa wananunua.

“Mambo siku hizi yamebadilika wanaume wengi wamekuwa wakipenda urembo kama wanawake tena husani urembo wa vipini vya puani, mara ya kwanza aliwahi kuja mteja wa kiume kuulizia hereni na vipini mimi nilijua huo urembo ni kwa ajili ya wanawake kumbe ulikuwa wa kwake, baada ya kumuona akivaa mbele yangu.

Basi kutoka hapo sikushangaa tena nikajua ni mambo ya fashion na utandawazi tunaoiga kutoka kwa wasanii wakubwa na watu maarufu duniani wanaoenda na wakati na dunia inavyotaka” alisema Sharifu.

Haya sasa mambo ya fashion hayo bado Sharifu anatoa maoni yake kuhusiana na urembo huo unachukuliwaje katika jamii.

“Unajua kwa maadili ya kwetu kidogo kumekuwa na ukakasi kuhusu wanaume kuingilia urembo wa wanawake lakini sisi watu wa fashion tunaona kawaida ni style ambazo zimezalishwa hivi karibuni kwa ajili ya kutafuta muonekano” alisema muuza urembo huyo.

Kama nilivyo kuambia hapo awali katika fashion kuna mambo mengi sana hivyo unapaswa kuielewa vizuri, waweza kushanga uvaaji wa urembo huu kama fashion kwa wanaume.Basi Mwananchi Scoop hakuishia hapo tukakutana na Mwanamvita maarufu kama Mama Abuu mkazi wa Dar es salaam, yeye ametoa maoni yake jinsi anavyo wachukulia wanaume wanaovaa vipini na hereni anaeleza kuwa maadili hayo zamani yalikuwa hayapo kwenye fashion kwa wanaume.

“ Utandawazi umekuwa ukiwapeleka vijana kwenye dunia nyingine kabisa hasa katika maswala ya fashion, kumekuwa kuna mambo ya tofauti kila siku.

Zamani wazee wetu walikuwa wakiwakataza watoto ama vijana kuvaa urembo wa vipini puani na kutoboa pua au masikio tofauti na sasa mambo ya mekuwa tofauti” alisema Mwanamvita.

Pia aligusia vijana kuiga uvaaji wa namna hiyo kwa wasanii na watu maarufu kitu ambacho kwa upande wake anaona kama siyo sahihi.

“vijana siku hizi wamekuwa wakiiga fashion kutoka kwa wasanii au watu maarufu kitu ambocho hawawazi kama kitakuwa na madhara au faida ilimradi waende na fashion”.

Hapa sasa kila mtu na mtazamo wake katika uvaaji wa vipini na hereni kwa wanaume lakini fashion na urembo kila mtu ana-choice yake ya kuchagua ni fashion gani aende nayo katika maisha yake.

Nikwambie tu kwa leo tukwamie hapo tukutane next week hapahapa kwenye magazine yetu, nikukumbushe usisaha kufatilia magazine ya Mwananchi Scoop ili uweze kupata tarifa za uhakika.

Hii imeenda!!!!!!!


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post