Uvaaji wa kisela unambeba Jux

Uvaaji wa kisela unambeba Jux

Jux hana muziki wa kutisha na kumekuwa na maneno mitaani kuwa anaimba ila siyo kwa kiwango cha juu.

Ndiyo hata yeye naamini anafahamu kuwa Mungu hakumbariki uwezo wa Q Chilla au Ben Pol. Lakini ana kitu cha ziada ambacho pia ni sehemu ya muziki.

Muonekano ni sehemu ya muziki. Hili liliwashinda kina Twenty Percent. Uvaaji wa kisela ilikuwa silaha wakati ule muziki wakiimbiwa masela zaidi. Ndipo watu sampuli ya Juma Nature walishika soko. Lakini hizi ni nyakati za kina Jux.

Dunia ya kujilipua kwa pamba na muonekano. Hapa ndiyo kwenye eneo tengefu kwa Jux. Kafanikiwa sana kwani anaongelewa kwa uvaaji kuliko uimbaji.

Kabla ya kipaji chake angalia aina ya mashabiki wake. Na anawanasa kwa lipi? Wengi ni ‘mademu’ na sumu yake kwao ni upigaji wa pamba na zaidi dawa ya 'demu' ni 'demu'.

Pisi kali kukaa kando ya Jux ni silaha nyingine. ‘mademu’ huvutiwa zaidi na msela mwenye 'mademu' wakali. Bila kuyaelewa haya, dunia itakuacha hapo hapo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags