Utani wa Diamond, Innossb kuhusu timu za taifa

Utani wa Diamond, Innossb kuhusu timu za taifa

Ikiwa yamebaki masaa machache kuelekea mchezo wa mwisho wa kundi F kupitia michuano ya #Afcon unaotarajiwa kuchezwa kesho kati ya Congo dhidi ya Tanzania wanamuziki Diamond na Innossb wameamua kutaniana kuhusiana na game hiyo ya kesho.

Ambapo mwanamuziki kutoka Congo Innossb ali-post picha iliyoambatanishwa na ujumbe usemao ‘siwezi kusubiri ukiwa unalia baada ya game kuisha’ huku Diamond akimjibu ‘Ni bora kupokea simu yangu baada ya mchezo kuisha’.

Wawili hao walishawahi kufanya ‘kolabo’ ya ngoma ya ‘Yope’ ambayo ilifanya vizuri kupitia mitandao ya kijamii, mpaka kufikia sasa imefikisha watazamaji zaidi ya milioni 200 kwenye mtandao wa YouTube huku ikiwa na miaka minne tangu kuachiwa kwake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags