Utafiti: Wanaolalia tumbo hatarini kukosa pumzi

Utafiti: Wanaolalia tumbo hatarini kukosa pumzi

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Dk Tony Nalda, kutoka katika kituo cha Scoliosis unaeleza kuwa wanaolalia tumbo hatarini kuathiri upumuaji kutokana na kukandamiza Diaphragm.

Tony anawaonya watu kulalia tumbo na kudai kuwa kunaweza kusababisha matizo mbalimbali kama vile ya shingo na mgongo, shida katika upumuaji pia kudhoofisha mfumo wa moyo na mishipa.

Aidha kupitia makala yake ameeleza kuwa unapolalia kifua na tumbo kunazuia kutiririka kwa damu katika moyo ambapo inaenda kuongeza hatari ya moyo hivyo kupelekea kupata shinikizo la juu la damu ambalo ni tatizo hasa kwa watu walio na hali ya awali ya ugonjwa wa moyo.

Hata hivyo alishauri baadhi ya njia salama za kulala ikiwa ni pamoja na kulalia mgongo na ubavu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags