Utafiti: Kumshika mkono umpendaye ni njia ya kunapunguza maumivu

Utafiti: Kumshika mkono umpendaye ni njia ya kunapunguza maumivu

Kwa mujibu wa Utafiti wa Pavel Goldstein kutoka chuo kikuu cha Colorado, Boulder, unaeleza kuwa kushikana mikono na mtu unayempena na kumjali kunauwezekano mkubwa wa kupunguza maumivu na kumfanya mtu kujisikia vizuri.

Uponyaji huo unakuja kutokana na miili ya watu hao wawili kuanza kufanya kazi kwa maelewano, hata hivyo utafiti huo umeeleza kuwa kushikana mikono ni zaidi ya njia ya kuonesha upendo inayoweza kusawazisha mapigo ya moyo, na hata kupunguza maumivu.

Hii ni kwa sababu ngozi ya binadamu imejaa neva inayoitikia mguso, ikitoa homoni za kujisikia vizuri kama vile ‘Oxytocin’, inayojulikana kama (Love Hormone) homoni ya upendo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags