Utafiti: aliyeishi chini ya maji siku 100 hatozeeka mapema

Utafiti: aliyeishi chini ya maji siku 100 hatozeeka mapema

Alievunja rekodi kwa kukaa chini ya maji kwa muda mrefu Dk. Joseph Dituri anadaiwa kuwa kukaa kwake chini ya maji kumemsababisha kutozeeka mapema.

Uchunguzi uliofanywa wakati alipokuwa chini ya maji ulieleza kuwa telomeres zake ambazo kwa kawaida hufupisha umri, zimeonekana kuwa ndefu kwa asilimia 20 kuliko hapo awali.

Hii imesababishwa na mazingira aliyokuwa akiishi chini ya maji ambapo imedaiwa kuwa chumba alichokua akiishi kina hyperbaric (ni hewa ambayo inakusaidia kupumua ‘oksijeni’ safi), hivyo basi vyumba kama hivyo husaidia kupunguza kasi ya kuzeeka.

Kutokana na hali hiyo, Dituri anaamini kuwa kukaa kwake chini ya maji kwa siku 100 kunaweza kuwa kumechangia kuleta nguvu mpya, na kumfanya ajione kama kijana mdogo.

Joseph Dituri kutoka nchini Marekani alivunja rekodi ya dunia ya Guinnesse kwa kuishi chini ya maji kwa siku 100, aliingia kwenye kitabu hicho Juni 2023. Kwa sasa Joseph ana umri wa miaka 56






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags