Kutokana na ugumu wa maisha, baadhi ya watu wameamua kujiajiri kwa kufungua biashara mbalimbali zinazoweza kuwaongezea kipato.
Kwa kulitambua hilo Mwananchi Scoop tumekusogezea mambo ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara, ili usikumbane na changamoto zozote zitazofanya uishie kati katika biashara yako.
- Utafiti wa Soko
Fahamu mahitaji ya wateja na upungufu uliopo sokoni. Usikurupuke kuanzisha kitu kwakuwa rafiki au ndugu yako ameanzisha biashara. Pia jitahidi kuchunguza washindani wako namna wanavyofanya kazi.
- Mpango wa Biashara
Kabla ya kuanzisha biashara yoyote unatakiwa kuandika mpango wa biashara ikiambatana na malengo, mikakati, gharama, faida unayotaka kuingiza kupitia biashara hiyo.
- Mtaji na Bajeti
Baada ya kupanga mpango wa kufanya biashara unachotakiwa ni kuhakikisha unapangilia bajeti zako kama vile gharama za uendeshaji, kodi, bidhaa na teknolojia yenye uwezo zaidi, na hii ni kutokana na biashara nyingi siku hizi kufanyika mtandaoni ambapo hapa utatakiwa kuwa na Simu kali, Lighligh na Bando la kutosha.
Usajili wa Biashara na Leseni
Hakikisha biashara yako inasajiliwa kisheria, unatakiwa kupata leseni na vibali vinavyohitajika iki kuepuka matatizo ya kisheria pamoja na kukimbizana na TRA.
- Mahali na Mfumo wa Uendeshaji
Chagua eneo sahihi kulingana na aina ya biashara yako, unachotakiwa kukifanya ni kuangalia kama sehemu unayo kwenda kufungua biashara yako je watu wa eneo hilo wanauhitaji wa biashara hiyo au umefungua ilimradi na wewe uonekane na biashara, ukifanya hivyo utapoteza pesa zako.
- Mkakati wa Masoko na Mauzo
Tengeneza mbinu za kuvutia wateja, kama matangazo na matumizi ya mitandao ya kijamii. Fahamu njia bora za kutoa huduma kwa wateja ili kuwawekea uaminifu na biashara yako.
- Uvumilivu na Kujifunza
Biashara inahitaji subira, juhudi, na uwezo wa kujifunza kutoka kwa changamoto. So unapoona maoni kwa mteja kuhusu bidhaa yako basi unatakiwa kujibu kwa nidhamu na adabu kwani unavyomjibu mteja mmoja vibaya kumbuka na wengine wanaona, kwahiyo jitahidi kuwa na kauli nzuri.
- Kujua jinsi ya kupambana na changamoto
Jua changamoto zinazoweza kutokea na jinsi ya kukabiliana nazo.Tafuta njia za kupunguza hasara, kama bima ya biashara.
Leave a Reply