Usichokijua kuhusu kinjunga na vijana

Usichokijua kuhusu kinjunga na vijana

Aisha Charles

Hellow!! my people once again tunakutana tena katika fashion hapahapa katika jarida letu pendwa la Mwananchi Scoop lengo letu sisi ni kukujuza yale yote yanayojiri katika fashion in and out wanetu sana.

Sasa leo katika fashion kuna jambo la tofauti kidogo hahahahahahahaa!!! manake hapo kwanza nicheke halafu wale wa kuvaa vinjunga tujuane hapa, maana tutaenda kujuzana usichokijua kuhusu kinjunga (kaptula) na vijana

Kinjunga  linaweza kuwa jina jipya masikioni mwako lakini katika tasnia ya mitindo ni vazi pendwa linalovaliwa na jinsi zote hasa rika la vijana wa kisasa.

‘Unavaa ‘kaptula’ au kinjunga una mguu wa kuvalia’ huu ni msemo ambao unapendwa kutumiwa na watu wengi wakiwa na maana ya vazi hilo huacha sehemu ya mguu wazi hivyo kuifanya miguu kuonekana vizuri sasa ndipo dhana ya una mguu wa kuvalia vazi hilo huja hapo.

Lakini katika tasnia ya mitindo vazi hilo halichagui jinsia ya kuvaa ila huvaliwa hasa na vijana. Lengo la makala haya ni kukupatia historia ya vazi hili na namna linavyo husianishwa na vijana wa leo. Bila kusahau namna unavyoweza kubamba na vazi hilo.

 Kinjunga au kaptula ni vazi la aina gani?

Kaptula au kinjunga ni suruali ya kipande yenye urefu unaoishia magotini na kukunjwa pindo. Vazi hili hupatikana katika aina mbalimbali za vitambaa hasa jeans.

Ni ipi asili na historia ya vazi la kaptula?

Kwa mujibu wa jarida la mitindo la ‘Old Bull Lee’ la nchini Uingereza, historia ya kaptula ni ya zamani zaidi mfano wa kwanza unaojulikana wa kaptula unaweza kupatikana mapema miaka ya 1800 katika sare za jeshi la ‘Nepali’.

Lakini, dhana ya kaptula za wanaume kama tunavyowajua leo ilizaliwa kwenye kisiwa cha Bermuda wakati wa vita vya kwanza vya kidunia.

Hii kwa kiasi kikubwa inatokana na ukweli kwamba kaptula zilizingatiwa kuwa hifadhi ya wavulana ambao walizitumia kama sare za shule za umma (serikali) na wakati mwingine kuwatenganisha na wanaume ambao umri wao umepevuka.

Katika kipindi hicho walihitaji kujisitiri na walihitaji nguo ndefu zaidi hivyo kuanza kuvaa suruali ili kuwatenganisha na vijana.

Siku za hivi karibuni vazi la kaptula au kinjunga limekuwa katika mtindo unaobamba si kwa jinsi ya kike au ya kiume na huvaliwa katika mtindo mbalimbali.

Vinjunga vilivyopo katika mitindo inayobamba ni vile vinavyokunjwa kwenye pindo usawa wa juu au chini ya magoti.

Muonekano wake kwa upande wa wanaume huwa vimeachia mwili tofauti na vinavyovaliwa na wanawake ambavyo wao pia hukunja chini lakini vinakuwa vimebana mwili.

Kwa nini vazi hili linahusianishwa na vijana?

Kuna baadhi ya mavazi katika jamii yetu ya leo yanaweza kuwatofautisha baadhi ya watu kulingana na rika pamoja na mazingira husika. Kwa kiasi kikubwa vazi la kinjunga kwa kipindi hiki limekuwa likivaliwa na vijana wengi kutokana na kuendana na wakati wa utandawazi unaoendana na ubunifu wa mavazi.

Hii ni kutokana na mtazamo wa wavaaji ambao hujiona wapo huru katika vazi hilo kwa sababu linawapa muonekano mzuri na kutokelezea zaidi.

Namna unavyoweza kutokelezea na vazi la kinjunga

Ili upate muonekano mzuri na wa kuvutia unapokuwa umevaa kinjunga hauna budi kuzingatia muktadha na aina ya nguo unazovalia vazi hilo, kwa upande wa jinsi ya kike, unaweza kuvalia na tisheti ambalo ni oversize au wakati mwingine crop top endapo hauna kitambi.

Hakikisha kinjunga chako ni highwest mpaka usawa wa tumbo ili kuzuia kuacha sehemu ya mwili wazi bila kusahau mashati ya makenzi ambayo yanabamba zaidi kwa chini ukavalia na raba zisizokuwa na rangi rangi, pia vinjunga unaweza kuvalia na sendo na ukapendeza zaidi.

Kwa upande wa jinsia ya kiume kinjunga unaweza ukavalia na tisheti, mashati ya mikono mirefu, mashati ya makenzi pia na wakati mwingine vesti.

Wabunifu wamavazi wanazungumziaje vazi hili?

Akizungumza na Mwananchi Scoop mbunifu wa mavazi  na fundi nguo Mkaile Jamal anasema vazi la kinjunga jina lake linatokana na mtindo wake unaotofautishwa na kaptula za kawaida kwa sababu vazi hilo huwa fupi na mtindo wake wa kukunjwa kwenye pindo. 

Ni vazi ambalo linawapa uhuru wavaaji hasa kulingana na mabadiliko ya tabia ya nchi joto kuongezeka kwa kiwango cha juu hivyo huwafanya wawe huru na kupata hewa. Anaeleza katika tasnia ya mitindo hamna kitu kipya ila ni uboreshaji tu na ubunifu.

“Siku zote mavazi yanaendana na wakati, zamani ulikuwa ukivaa kaptula fupi unaonekana upo uchi lakini ulimwengu wa sasa na tasnia ya mitindo vazi hilo lipo katika trend na hasa msimu huu wa joto hauwezi kulikwepa, na vijana ndiyo wavaaji wakubwa” alisema Mkaile

Wavaaji wamelipokeaje?

Jackson Livingstone, anasema kinjunga siyo vazi jipya ila ni ubunifu umefanyika lakini limepokelewa na kuvaliwa sana changamoto kuna baadhi ya maeneo huwezi kuvaa hasa yale yenye baridi kali kama Mbeya, Iringa.

“ Hata kama unataka kufa na ‘fasheni’ lakini ukiwa sehemu kama Makambaku Iringa huko unapata wapi ujasiri wa kuvaa kinjunga na kama utavaa mara chache sana ila hilo vazi linabamba sana.” Anasema Jackson

Kwa upande wa wazazi na jamii wanasemaje?

Frola Kambaulaya maarufu kama mama Imma anaeleza kuwa kuna wakati kama wazazi wanajitahidi kukubaliana na utandawazi ila tasnia ya mitindo itaendelea kukua kila siku.

Anashauri  wanapovaa vinjunga wazingatie mazingira kuna sehemu kama nyumba za ibada na maofisi ya umma inawazuia kuvaa kutokana na maadili. Hivyo ni vyema kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.

“Kuna wakati nimepiga kelele kwa wanangu kuhusu hivyo vunjunga lakini nikiingia mitandaoni naonaa watu wengi wanavaa na rika ndiyo hilohilo la vijana wangu. Mimi huwa nawakubalia wavae lakini siyo wakienda katika ibada na maofisini” Anasema Frola.

Haya sasa kama ilivyo ada huwa atuchoshani sana tuna elimishana na kujuzana kuhusu fashion, mimi nikwambie tu till next time.

 

Hii imeenda!!!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags