Upinzani wasusia matokeo yaliyoanza kutolewa, Nigeria

Upinzani wasusia matokeo yaliyoanza kutolewa, Nigeria

Chama kikuu cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP) na Labour Party vimedai hakuna uwazi katika mfumo mpya wa kielektroniki wa wapiga kura.

Vyama vya upinzani vimetoka nje ya ukumbi ambapo matokeo ya uchaguzi wa rais wa Nigeria wenye upinzani mkali yanatangazwa.

Huu ni uchaguzi wa kwanza wa kitaifa ambapo kifaa cha kielektroniki kimetumika kuwaidhinisha wapiga kura.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (Inic) Mahmood Yakubu alisema utangazaji wa matokeo utaendelea hata hivyo tume hiyo imekanusha malalamiko ya vyama vya upinzani.

Mwakilishi wa PDP katika kituo cha uchaguzi huko Abuja alielezea mchakato huo kuwa wa udanganyifu, na kushutumu chama tawala cha All Progressives Congress (APC) kwa kushirikiana na IEC, huku chama cha Labour kikiomba kusitishwa kwa matangazo hayo, au uchaguzi kufutwa na kurudiwa upya.

Chama cha APC ambacho mgombea wake Bola Tinubu amepata uongozi wa mapema kutokana na matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa, kimesema kwamba wale ambao hawajaridhika na matokeo hayo waende mahakamani, na vyama hivyo viache kwanza mchakato huo uendelee.

Takriban thuluthi moja kati ya majimbo 36 yakitangazwa rasmi, Tinubu ana asilimia 44 ya kura zilizopigwa, mbele ya Abubakar kwa 33%, na Obi kwa 18%.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post